Kurasa za mwisho za De Gea Manchester United

MLINDALANGO wa Manchester United, David de Gea anatarajiwa kuondoka ndani ya timu hiyo mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa mwezi Juni 2023.

Taarifa kutoka vyombo mbalimbali vya habari barani Ulaya zimeeleza kuwa De Gea ameshindwa kukubaliana na Manchester United ili asaini mkataba mpya ambapo United wanamtaka kipa huyo kupunguza mshahara lakini wamegonga mwamba.

De Gea mwenye miaka 32 ameitumika Manchester United kwa miaka 12 tangu alipojiunga nao mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid ya Hispania.

Advertisement

David de Gea ameichezea miamba hiyo ya jiji la Manchester United michezo 545 na kuondoka na hati safi ( Clean sheet) 190.

Klabu mbalimbali kutoka mataifa ya Uarabuni zinahusishwa kuitaka huduma ya Degea atakapoamua kuachana na Manchester United.