Kuzaa watoto wengi kunaweza kusababisha saratani ya mlango wa kizazi

WATAALAMU wa afya wameeleza sababu kubwa ya wanawake kupata saratani ya mlango wa kizazi ni ngono katika umri mdogo na wanawake kuzaa watoto wengi.

Sababu zingine zilizotajwa wanawake kuwa katika hatari ya kupata saratani hiyo ni wanawake  wanaofanya ngono na wanaume wengi na wale wenye virusi vya UKIMWI.

Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Muuguzi, Rajabu Matembo, wakati  wa kongamano linalohusu watumishi wanawake wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili-Mloganzila.

Kutokana na hilo jamii imeshauriwa kufanya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi mapema ili kuweza kujikinga na ugonjwa huo, kwani ukibainika mapema unaweza kutibiwa na kupona kabisa.

Mkuu wa Idara ya Huduma za Ukunga na Afya ya Mama na Mtoto wa hospitali hiyo, Zuhura Mawona amesema kuwa kutokana na tafiti zilizotolewa GLOBOCAN mwaka 2018 na inaonesha kuwa wanawake 570,000 waliugua saratani ya mlango wa kizazi na kati yao 311,000 walipoteza maisha.

Vilevile amebainisha kuwa mwaka 2018 alifanya utafiti mdogo kwa wauguzi wa MNH na wauguzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, ambapo kati ya 323 asilimia 11.

8 pekee ndio waliofanya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi.

“Ugonjwa huu hauna dalili mtu atakaa nao kwa muda mrefu zaidi na pale anapopata wazo la kwenda kupima baada ya kuona dalili unakuta ugonjwa umeshakua endelevu na mtu anaweza kupoteza maisha na matibabu yake yanakuwa ni gharama zaidi,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button