WANANCHI mbalimbali, leo wamejitokeza kumzika mfanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Zaituni Saedia, aliyefariki usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.

Zaituni amezikwa jioni hii katika makaburi ya Bakwata, Kinondoni, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wafanyakazi wenzake wa TSN, majirani, ndugu na jamaa.