Laini za simu, miamala yaongezeka

DAR ES SALAAM: WIZARA ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (HMTH) imeelezea kuwa na ongezeko la usajili wa laini za simu na miamala ya kifedha katika kipindi cha mwaka mmoja kilichoanza April, 2022 hadi Aprili 2023.

Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohamed Khamis Abdulla akizungumza jijini Dar es Salaam amesema kuna ongezeko la usajili wa laini za simu za mkononi kutoka milioni 55.7 mwezi Aprili 2022 hadi milioni 62.1 mwezi Aprili 2023, ikionyesha ongezeko la asilimia11.8.

Pia amesema, watumiaji wa huduma za pesa kupitia simu za mkononi wameongezeka kwa asilimia 24.1, kutoka milioni 35.7 hadi milioni 44.3.

“Watumiaji wa mtandao wa intaneti wameongezeka kutoka milioni 29.9 hadi milioni33.1, ikiashiria ongezeko la asilimia10.7,” amesema Abdulla na kuongeza.

“Maendeleo haya yanathibitisha kuwa tuko katika mwelekeo sahihi kwenye uchumi wa kidijitali, “amesema.
Aidha, amesema, serikali imekamilisha Rasimu ya Mkakati wa Uchumi wa Kidijiti wa Kitaifa Tanzania Digital ‘Economy Framework’ kwa kipindi cha Mwaka 2023-2033, ikiwa inangojea idhini ya mwisho.

“Mafanikio ya mkakati huu ni kutokana na ushirikiano wa wadau mbalimbali kutoka Sekta binafsi na Sekta ya Umma kupitia vikao vya kiufundi vilivyoratibiwa na Wizara yetu, “amesema.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Angila
Angila
25 days ago

I have just received my 3rd paycheck which said that $16285 that i have made just in one month by working online over my laptop. This job is amazing and its regular earnings are much better than my regular office job. Join this job now and start making money online easily by
.
.
.
.
Just Use This Link……..> > > http://Www.Smartcareer1.com

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x