Laini za simu milioni 72.5 zimesajiliwa

DODOMA: WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Sekta ya Mawasiliano imeendelea kukua ambapo takwimu zinaonesha laini za simu zilizosajiliwa zimeongezeka kutoka milioni 62.3 Mwezi Aprili, 2023 hadi kufikia laini milioni 72.5 Mwezi Aprili, 2024 sawa na ongezeko la asilimia 16.4.

Waziri Nape, ameyasema hayo wakati akiwasilisha Makadirio ya Bajeti yake kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 leo Mei 16,2024 bungeni jijini Dodoma.

“Watoa huduma wa miundombinu ya mawasiliano wamefikia 25 ukilinganisha na watoa huduma 23 Mwezi Aprili, 2023 sawa na ongezeko la asilimia 8.7,” amesema Waziri Nape.

Soma pia: https://habarileo.co.tz/laini-za-simu-miamala-yaongezeka/

“Takwimu zinaonesha wastani wa bei ya dakika ndani ya mtandao bila kifurushi (Shilingi/Dakika) zimeendelea kushuka kutoka Sh 29 mwezi Juni, 2023 hadi kufika wastani wa Sh 26 Aprili,2024 wakati bei ya dakika nje ya mtandao bila kifurushi imeshuka kutoka wastani wa Sh 31 kwa Juni, 2023 hadi kufikia wastani wa Sh 28 kwa Machi 2024,” amesema Waziri Nape.
Soma pia: https://www.tcra.go.tz/download/sw-1619108384-October-%20December%202019%20Edition.pdf

Habari Zifananazo

Back to top button