LATRA waongeza wiki mbili maoni kuhusu kanuni

MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeongeza muda wa wiki mbili kwa wadau wa usafiri nchini ili kuweza kutoa maoni yao katika kanuni za Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini za utaratibu wa kushugulikia malalamiko ya mwaka 2023.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa huduma za usafiri,Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi,Sekta ya Uchukuzi  mhandisi Aron Kisaka wakati wa mkutano wa kupokea maoni ya wadau kuhusu rasimu  za kanuni mpya za mamlaka.

Kisaka amesema  kanuni  zimechelewa kuwafikia wadau na siku bado hazitoshi kwa wadau wa usafiri kuweza kutoa maoni yao. Amewaomba  wadau wa usafirishaji nchini waweze kutuma maoni yao kwa barua pepe ili isaidie katika ukusanyaji wa maoni.

Advertisement

Naye Mkurugenzi wa udhibiti wa Usafiri wa barabara kutoka LATRA, Johansen Kahatano amesema Mamlaka yao itaendelea na ukaguzi wa lazima wa vyombo vya usafirishaji Biashara kwa mwaka 2023.

Amewashauri watumiaji wa usafiri kupanda mabasi yalio salama. Amesema ukaguzi wa magari ya biashara  utahusisha watalam kwa kutumia mitambo ya kisasa ya ukaguzi.