LATRA yatangaza ruti mpya 10 daladala Dar

DAR ES SALAAM: MAMLAKA ya Usafiri wa Ardhini (LATRA) imetangaza ruti mpya 10 za daladala zitakazoanzia katika Kituo kipya cha Mwenge, jijini Da es salaam

Taarifa ya LATRA kwa umma hii leo, imeoredhesha ruti hizo kuwa ni, Mwenge kwenda Mbande Kisewe kupitia Barabara ya Mandela, Kilungule.  Mwenge kwenda Buza kutumia Barabara ya Mandela, Usalama.

Katika ruti hizo zinazopitia Barabara ya Mandela ni  Mwenge kwenda Sigara Sokoni, Mwenge kwenda Tabata Kimanga na Mwenge kuelekea Tabata Segerea.

Ruti ya Mwenge kwenda Kigogo Sokoni, Barabara zitakazotumika ni Mandela, Nyerere. Mwenge kuelekea Madale, kupitia barabara ya Makongo. Mwenge kuelekea Stesheni itatumia Barabara ya Bagamoyo, Ally Hassan Mwinyi, Bibi Titi.

Ruti ya Mwenge kuelekea Mnazi Mmoja kupitia Barabara ya Mandela, Uhuru na Mwenge kuelekea Mnazi Mmoja itatumia Barabara ya Mabibo, Kawawa, Uhuru.

LATRA imewataka wenye daladala kuomba ruti hizo na imetaja vigezo vya kuzingatia kwa wamiliki wa magari yenye usajili kuanzia namba DXA kwa njia ya kuanzia na kuishia Stendi mpya ya Mwenge  na kwa gari jipya ambalo halijawahi kusajiliwa katika mfumo wa utoaji wa leseni  wa PRIMS dereva wa gari anapaswa kuthibitishwa LATRA.

Sare za madereva na makondakta ni suruali yenye rangi nyeusi na shati la mikono mifupi yenye rangi ya bluu bahari.

Habari Zifananazo

Back to top button