MAREKANI; LAURA Jeanne Reese Witherspoon ni msanii wa Marekani mwenye kipaji cha uigizaji, aliyezaliwa Machi 22, 1976 katika Hospitali ya Southern Baptist, New Orleans, Louisiana.
Dada huyu anajulikana kwa kazi zake kwenye filamu na tamthilia, pamoja na uongozaji na utayarishaji wa miradi mbalimbali ya filamu.
Witherspoon ameshinda tuzo kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja na Tuzo ya Academy,Primetime Emmy na tuzo mbili za Golden Globe.
Amekuwa miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani kati ya miaka 2006 na 2015, na ametajwa kwenye orodha ya wanawake 100 wenye nguvu zaidi duniani na Forbes katika miaka ya 2019 na 2021.
Pia mwaka 2021, alitajwa kuwa muigizaji anayelipwa zaidi duniani na thamani yake ilikadiriwa kuwa zaidi ya dola milioni 440 mnamo 2023.
Kazi ya uigizaji ya Witherspoon ilianza akiwa kijana mdogo, na amepata umaarufu mkubwa kwa mchango wake katika tamthilia kama “The Man in the Moon” na miradi mingine.
Filamu zingine kama “Tracy Flick,” “Elle Woods” kutoka “Legally Blonde,” na “Sweet Home” zilimsaidia kujipatia sifa kubwa katika tasnia ya uigizaji nchini Marekani na kushinda tuzo nyingi za uigizaji.
Nje ya uigizaji, Witherspoon amejihusisha na kutayarisha maudhui ya luninga yanayolenga kuelimisha juu ya masuala yanayowahusu wanawake chini ya kampuni yake ya Hello Sunshine. Pia ni mmiliki wa Klabu ya Vitabu ya Reese na kampuni ya mavazi, Draper James, na amejitolea katika mashirika ya utetezi wa haki za watoto na wanawake.
Kama mwanachama wa bodi ya Hazina ya Ulinzi ya Watoto (CDF) na Balozi wa Kimataifa wa Bidhaa za Avon tangu 2007,
Witherspoon ameendelea kusimama kidete katika kutetea haki za wanawake na watoto ulimwenguni kote.
Tunamtakia heri ya siku ya kuzaliwa Laura Jeanne Reese Witherspoon, ambaye leo anatimiza miaka 48.