Lebron aweka rekodi NBA

‘POWER Forwad’ wa timu ya mpira wa kikapu Los Angeles Lakers, Lebron James amekuwa mchezaji wa kwanza wa NBA kufikisha pointi 40,000.

Lebron amefikia idadi hiyo baada ya kupiga pointi 29 katika mchezo wa leo usiku dhidi ya Denver Nuggets.

Nyota huyo alikua kiongozi wa wafungaji bora wa muda wote wa NBA zaidi ya mwaka mmoja alipompita nyota wa zamani wa Lakers Kareem Abdul-Jabbar katika mchezo wa nyumbani dhidi ya Oklahoma City Thunder mnamo Februari 7, 2022.

Abdul-Jabbar alikuwa na pointi 38,387 katika misimu 20.

James aliingia kwenye mchezo wa Jumamosi akiwa na wastani wa pointi 27.1 kwa kila mchezo zaidi ya mashindano 1,474 katika misimu 21 ya NBA.

Habari Zifananazo

Back to top button