BREAKING: Klabu ya Leicester City ya nchini England imeshuka daraja rasmi, licha ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya West Ham United.
–
Leicester imeungana na Leeds kuelekea ligi ya Champions Ship, timu hizo mbili zimekamilisha idadi ya timu tatu ikiwemo Southampton ambazo zote zimeshuka daraja.
–
Almanusura Everton afuate mkumbo huo, ila ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bournemouth umemuokoa na kufikisha pointi 36 na kumuacha Leicester akiwa na 34, Leeds 31 na Soton 25.
Msimu wa Ligi Kuu England 2022/2023 umemalizika rasmi leo, Manchester City, Arsenal, Man United na Newcastle United wamefuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya na Leicester City, Soton na Leeds wameshuka daraja.