Lema amuomba Rais Samia kurejeshwa tanzanite Arusha

MWENYEKITI wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema amemuomba Rais Samia Suluhu kurejesha biashara ya madini ya Tanzanite ili ifanyike katika Jiji Arusha.

Lema amesema hayo leo Machi 4, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa lengo ni kukuza uchumi, ajira na biashara ya madini hayo

Mbunge huyo wa zamani wa Arusha Mjini amesema kuwa kuzuia kuuzwa nje ya Mererani madini ya Tanzanite ni kinyume cha sera ya biashara huria lakini pia kunadhofisha biashara hiyo.

Advertisement

“Mimi ushauri wangu ni kwamba, madini ya Tanzanite yauzwe kokote duniani na isionekane ni aina ya madini yanayonunuliwa na wazungu pekee”.amesema Lema.

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa Julai 7, 2021 wakati akizindua Kituo cha Tanzanite -Magufuli Mererani, alitangaza biashara ya Tanzanite kufanyika Mererani pekee ikiwa ni mkakati wa kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo.