Lemutuz kuagwa kesho Karimjee

MWILI wa Mmilimki wa Lemutuz Blog, William Malecela utaagwa kesho kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Lemutuz,  ambae alikua na matatizo ya moyo na alikua akipata matibabu yake katika hospitali ya Moyo ya Jakaya Kikwete amefariki dunia leo asubuhi na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Msemaji wa familia,  Kinjekitile Kingunge ‘Kinje’ akizungumza amesema, Lemutuz ataagwa Karimjee na mwili utasafirishwa kwenda Mvumi  Dodoma  kwa mazishi siku ya Jumatano saa tisa mchana
Amesema, kifo cha Lemutuz kimekua cha gafla  licha ya kusumbuliwa maradhi ya moyo alikua akiendelea vizuri hadi jana jioni alikua mwenye afya na furaha tele.
“Ndugu yetu alikuwa na matatizo ya moyo lakini alikuwa yuko vizuri tu, hadi jana usiku alikuwa mzima, ghafla leo alfajiri alijisikia vibaya, kakimbizwa hospitali ndio hivyo tena.”Amesema
Amesema, kwa sasa wanamsubiri baba wa marehemu  mzee John Malecela ambae yupo safarini na ataingia Dar es Salaam muda wowote kuanzia sasa ndio taratibu nyingine za mazishi zitaendelea.
“Lakini maziko yake yatafanyika Dodoma, Mzee akishafika ndio tutatoa ratiba kamili ya kumpumzisha ndugu yetu kwenye nyumba yake ya milele.  Amesema.
Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *