Leseni za madini mkakati zatoka

DAR ES SALAAM: Katika  kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassani  leseni za uchimbaji mkubwa wa madini mkakati zimetolewa.
Pia serikali imeliwezesha Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kununua mitambo mitano  ya uchorongaji  kwa ajili ya kuwahudumia wachimbaji wadogo na  imesambazwa katika maeneo ya Itumbi  Chunya, Lwamgasa Geita, Katente Bukombe, Buhemba Butiama na Dodoma.
Akizungumzia mafanikio ya sekta ya madini katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia, leo Machi 14, 2024 Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema ifikapo Juni 2024 mitambo yote itafikia idadi ya 15.
Aidha, amesema idadi ya Watanzania walioajiriwa kwenye migodi imeongezeka kutoka 14,308 kati ya waajiriwa wote 14,742 sawa na asilimia 97 kwa mwaka 2021 hadi kufikia ajira 18,580 kati ya 19,165 sawa asilimia 97 hadi kufikia Februari 2024.
Amesema, kwa mwaka 2023 jumla ya Dola za Marekani Bilioni 1.65 zilitumika kununua bidhaa na huduma kwa Kampuni za madini nchini.
Aidha, manunuzi ya  huduma na bidhaa kwa kampuni za Kitanzania yameongezeka kutoka Dola za Marekani Milioni 713 ambayo ni sawa na asilimia 82 ya manunuzi yaliyogharimu kiasi cha Dola za Marekani Milioni 874 kwa mwaka 2021 hadi kufikia dola za Marekani b
Bilioni 1.43 ambayo ni sawa na asilimia 86 ya kiasi cha Dola za Marekani Bilioni 1.65 ya manunuzi yote yaliyofanyika mwaka 2023.

Habari Zifananazo

Back to top button