Libya yatangaza hali ya dharura

SERIKALI ya Libya imetangaza hali ya dharura ya mwaka mzima kwa lengo la kuzuia kuenea magonjwa ya kuambukiza katika maeneo yaliyokuumbwa na mafuriko ya Mashariki mwa nchi hiyo.

Wiki iliyopita, kimbunga cha “Daniel” kilipiga maeneo kadhaa ya miji ya Benghazi, Al-Bayda, Marj, Susa, Shahatt na Derna.

Shirika la Afya Duniani lilionya kuhusu kuenea magonjwa ya kuambukiza katika maeneo yaliyokumbwa na kimbunga na mafuriko hayo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, Haidar al-Sayeh, mkuu wa Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Magonjwa nchini Libya, alitoa taarifa na kutangaza idadi ya sumu ambazo zimeripotiwa kutokana na matumizi ya maji ya kunywa huko Derna, Libya.

Akizungumzia kutotumika maji ya kunywa katika jiji la Derna, Al-Sayeh amesema kuwa, hali ya hatari ya mwaka mmoja itatangazwa katika maeneo yaliyoathiriwa na dhoruba na mafuriko.

Habari Zifananazo

Back to top button