LIGI Kuu ya Zanzibar msimu wa mwaka 2022/23 inatarajiwa kuanza Septemba 2 mwaka huu. Ligi hiyo inayoshirikisha timu 16 inatarajiwa kumalizika Juni mwakani.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na bodi ya ligi ya Shirikisho la Soka Zanzibar, (ZFF) jana, siku hiyo kutakuwa na mchezo mmoja kati ya Black Sailor na Malindi.
Mechi hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Amaan na inatarajiwa kuwa kali kwani mara ya mwisho kukutana msimu uliopita, Malindi ilifungwa mabao 5-0.
Aidha ratiba hiyo inaonesha kwamba Septemba 3 kutakuwa na michezo miwili kati ya Kipanga dhidi ya Zimamoto na KMKM dhidi ya Kundemba.
Siku inayofuata kutakuwa na michezo mitatu ambapo JKU itacheza na Uhamiaji, Polisi na Dula Boys na Finya Chipukizi itaikaribisha Mlandege.