Ligula wafanya upasuaji wa kihistoria

HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara-Ligula, imefanya upasuaji wa kihistoria  wa ukarabati wa mrija wa mkojo ‘Urethroplasty’ kwa mgonjwa aliyeonekana na tatizo la kuziba kwa mrija wa mkojo.

Upasuaji huo ni mara ya kwanza  kufanyika  hospitalini hapo ulifanywa na madaktari bingwa wa Mama Samia walioweka kambi maalum wakishirikiana na madaktari wa hospitali hiyo.

Akizungumzia tukio hilo Dk Hussein Msuma kutoka Hospitali ya Rufaa Temeke,  amesema kuwa upasuaji huo umempunguzia gharama mgonjwa huyo kusafiri kufuata huduma hiyo mkoani Dar es Salaam.

Advertisement

“Upasuaji huu umempunguzia gharama kubwa baada ya kuja kuhudhuria hapa katika kambi hii maalumu ya uboreshaji wa huduma za afya nchini ambayo ni kambi ya madaktari bingwa wa Mama Samia,” amesema Dk Msuma.

 

 

 

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *