Linah mbioni kurudi shule

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa Bongo Flava, Linah Sanga amesema anafikiria kurudi shule ya muziki ili kuongeża uwezo na kuendana na ushindani uliopo.

Akizungumza na mwandishi wetu, msanii huyo amesema kwa muda ambao amekuwa kimya ameona ushindani uliopo hivyo ili aweze kuendana nao ni vyema akarudi darasani kuboresha baadhi ya vitu.

Msanii huyo amesema kutokana na uzoefu aliokuwa nao anaamini itamchukua miezi mitatu hadi miwili kukaa sawa kabla ya kurudi kwenye gemu ambayo anaamini atarudi kwa kasi na kuwarudisha mashabiki zake ambao kwa muda mrefu hawajamuona akipanda jukwaani.

Amesema katika kipindi hiki pia atajitahidi kuwa karibu na rafiki zake wa muda mrefu, Amin Mwinyimkuu ‘Amini’ na Elias Barnaba ‘Barnaba Classic’ ili kukumbushia baadhi ya vitu ambavyo walijifunza wakati huo wakiwa kituo cha Tanzania House of Talent (THT) chini ya marehemu Ruge Mutahaba.

Linah ni miongoni mwa wasanii wa kike maarufu nchini aliyetamba na wimbo wake wa wrong number ambao alishirikiana na Barnaba.

Habari Zifananazo

Back to top button