“Lindi, Mtwara tunatarajia mradi mkubwa wa gesi”
MTWARA: RAIS Samia Suluhu Hassan amesema barabara na miundombinu yote ambayo itahusika na mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia (LNG) mkoani Lindi itaanza kujengwa utekelezaji wa mradi huo utakapoanza.
–
Rais amesema hayo leo wakati akionge na wananchi wa kata ya Nanguruwe, Mtwara Vijijini mkoani Mtwara.
–
“Lindi na Mtwara tunatarajia mradi mkubwa sana wa gesi, ule mradi utakapokuja barabara zote zinazohusiana na mradi ule zinakwenda kujengwa.” amesema.
–
Rais amesema kwa sasa serikali ipo kwenye hatua za mwisho za mazungumzo ili mradi wa LNG uanze kujengwa.
–
Raisi Samia Suluhu Hassan yupo Mtwara kwa ziara ya siku nne kukagua miradi ya maendeleo, kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
–