Lindi, Mtwara wapewa somo kushirikiana na Ewura

MTWARA; Maofisa Biashara wa Halmashauri za Mikoa ya Lindi na Mtwara, wametakiwa kufanya shughuli zao kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Nchini (Ewura).

Akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo maofisa hao kuhusu kufahamu, shughuli zinazofanywa na Ewura, Meneja wa Kanda ya Mashariki Nyirabu Musira amesema kutokana na wao kuwa na majukumu mengi hususani kanda hiyo inafanya kutokuwepo kila sehemu kwa wakati.

Amesema ni imani yake kuwa mafunzo yatakuwa yenye tija kwao, huku lengo la mafunzo likiwa ni pamaoja na kuwawezesha maofisa hao kufanya shughuli zao kwa kusaidiana na Ewura mkoani Mtwara.

“Kutokana na kuendana na shughuli ambazo wanazifanya na kupata mafunzo, itawasaidia maofisa biashara kuwa mkono wa Ewura pale ambapo watakuwa hawajafika kwenye maeneo husika,”amesema Musira

Amesema sasa wameanza kuchukua hatua kwa wafanyabiashara ambao wamekuwa wakificha taarifa, na ambao hawawasilishi taarifa zao katika mfumo unaopaswa kutumika.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Dk. Stephen Mwakajumilo ametaka pande hizo zote mbili kujadiliana kwa pamoja, namna ya kutatua changamoto zinazojitokeza kwenye sekta ndogo ya mafuta.

Habari Zifananazo

Back to top button