Lindi wapongeza uwepo maji ya uhakika

WAKAZI wa Kata za Nyangao, Mtama, Majengo, Kitomanga, Madangwa wilayani Lindi wameanza kutumia maji yanayotokana na bomba.

Katibu wa Kamati ya Watumiaji maji kutoka kata hizo, George Kalmaga akizungumza na HabariLEO amesema  baadhi ya wakazi tayari wameshawekewa maji kwenye nyumba zao na kupongeza serikali kwa hatua hiyo.

Amesema mabadiliko hayo yanatokana Wakala wa Majisafi na Usafi za Mazingira Vijijini (Ruwasa) kuweka miundombinu kipindi hiki cha miaka minne.

Amesema kabla ya uboreshaji huduma hiyo, walikuwa wanapata maji katika mto Nyangao,  ambayo hayakuwa salama kwao kwa kunywa, kupikia na matumizi mengine ikiwemo kuoga na kufulia.

“Sasa maji yanapatikana chanzo cha mto Chiule na kuhifadhiwa katika tenki la maji na kuwekwa dawa, kisha kusambazwa,” amesema.

Mkazi wa Kata ya Kitomanga wilayani Lindi, Asia Nango amesema wananchi sasa wana uelewa wa kutosha juu ya maji yatokanayo na bomba na yale ya mito ya kawaida ambayo walikuwa wakichangia na wanyama.

Habari Zifananazo

Back to top button