Lineker asimamishwa uchambuzi

MTANGAZAJI wa kipindi cha michezo cha ‘Match of the day’ cha uchambuzi wa soka kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la BBC, Gary Lineker amesimamishwa kufanya kipindi hicho baada ya kukosoa sera ya uhamiaji na wahamiaji haramu wanaoingia nchini Uingereza kwa kusema sera hiyo ni ya kikatili.

Gary Lineker ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa timu ya Taifa ya England na klabu ya Barcelona alitumia akaunti yake ya Twitter kukosoa sera hiyo ambayo imeendelea kuzua gumzo nchini humo.

Baada ya kusimamishwa kutangaza kipindi hicho mpaka atakapopewa taarifa nyingine baadhi ya wachambuzi wenzake ambao pia ni magwiji wa England, Alan Shearer na Ian Wright wamesema hawatofanya uchambuzi.

Advertisement

Hatua hiyo inapelekea michezo ya EPL ya leo kurushwa bila wachambuzi kwa upande wa shirika hilo.

/* */