Lingard atambulishwa Korea

SEOUL, Korea Kusini: MSHAMBULIAJI raia Uingereza, Jesse Lingard amejiunga na klabu ya Seoul FC kwa uhamisho huru.

Lingard (31) ametambulishwa jana na wababe hao wa Korea Kusini kwa kandarasi ya miaka miwili. Amekuwa huru tangu kuachana na Nottingham Forest ya England mwaka jana.

Akiwa Forest msimu wa 2022-23 alishuka dimbani mara 17, isivyo bahati hakutikisa wavu.

Lingard amepikwa na kutambulika zaidi katika ulimwengu wa mpira wa miguu akiwa na mashetani wekundu, Manchester United ya England.

Amehudumu United tangu mwaka 2011-2022, ingawa mara kadhaa amekuwa akitolewa kuhudumu kwa mkopo katika vilabu kadhaa nchini humo vikiwemo Leicester City, Birmingham City, West Ham United, Brighton and Hove Albion na vinginevyo.

Akiwa United, amefanikiwa kutwaa mataji kadhaa yakiwemo UEFA Europa League, FA Cup, Ubingwa wa Ligi Kuu England (EFL) na Ngao ya Jamii.

Habari Zifananazo

Back to top button