Lishe duni, wapenzi wengi huathiri nguvu za kiume

IMEELEZWA kuwa changamoto kubwa ya upungufu wa ngumu za kiume ni lishe duni wanayotumia wanaume na kuwa na wapenzi wengi.

Aidha, changamoto nyingine ya upungufu wa nguvu za kiume ni msongo wa mawazo na mtindo wa maisha.

Hayo yalisemwa mjini Kibaha na Mganga Mkuu wa Wilaya Halmashauri ya Mji Kibaha, Tulitweni Mwinuka.

Mwinuka alisema changamoto kubwa ya upungufu wa nguvu za kiume unatokana na lishe duni hali ambayo inasababisha upungufu huo kwani hawali vyakula vya kujenga mwili.

“Ni kweli kuna tatizo kubwa la nguvu za kiume lakini sababu kubwa ni lishe duni, watu wanahangaika bila ya kuwa na lishe nzuri changamoto, hii haiwezi kuisha,” alisema.

Alisema changamoto nyingine ni wanaume kuwa na wapenzi wengi hivyo kushindwa kuwamudu.

“Pia kuna ugonjwa wa kisukari nao unachangia tatizo hilo, hivyo watu wanapaswa kwenda hospitali badala ya kwenda kwa waganga wa kienyeji ili wapatiwe matibabu wakati mwingine ni msongo wa mawazo tu na hakuna haja ya kutumia dawa bali ni ushauri tu,” alisema.

Alibainisha kuwa wanandoa wanapaswa kuzingatia suala la lishe kuanzia kwa vijana na hata watu wazima na kuacha kuwa na wapenzi wengi wakati lishe ikiwa duni.

“Tunasisitiza lishe kuanzia inapotungwa mimba, mtoto anapotengenezwa yaani siku 1,000 hadi mtoto anapofikisha miaka miwili kwani suala hilo linaanzia kwenye ubongo,” alisema.

Aliwataka watu wazingatie lishe na kula vyakula vya kujenga mwili, milo kamili ikiwa ni pamoja na ulaji wa matunda, kuachana na matumizi ya uvutaji sigara.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x