Lissu ashangaa gari alilopigwa risasi

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu kwa mara ya kwanza ameshuhudia gari lake aliloshambuliwa nalo Septemba 7, 2017 likiwa na matundu 30 ya risasi na kumpa mshtuko kama yupo hai mpaka leo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dodoma leo, Lissu amesema baada ya kufika kituoni hap oleo, polisi walimpa fursa ya kuliona gari lake alilokuwa akilitumia siku aliyoshambuliwa na kujeruhiwa.

“Nimekuwa nikiwasiliana na polisi kwa muda mrefu kuhusiana na kuja kuliona gari langu, lakini kutokana na majukumu yao, leo wamenipa nafasi ili kuliona…yani nimehesabu yale matundu ya risasi nimeyaona 30, hii ni hatari sana,” amesema Lissu mbele ya wanahabari.

Hata hivyo, Lissu amesema kwa sasa anafanya utaratibu wa kulitoa gari hilo polisi, kwani kwa sasa haliwezi kutembea zaidi ya kubebwa na gari kubwa.

Habari Zifananazo

Back to top button