Lissu ashauri mfumo wa kodi uboreshwe
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema kuna haja ya kuboresha mfumo wa ukusanyaji wa kodi nchini, ili kuwepo uwiano baina ya wafanyabiashara haswa katika kupata faida.
Lissu ameyasema hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaam leo Julai 5, 2023.
Amesema wanaokusanya kodi lazima wawe wasafi, ili waisadie serikali kupata kodi kiuhalali na iweze kulinganisha hali halisi ya biashara za wafanyabiashara nchini