Liverpool kuwakosa watano

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp ameorodhesha orodha ya wachezaji majeruhi ambao watakosa michezo kadhaa ya timu hiyo ya Ligi Kuu.

Klopp amesema mshambuliaji Diogo Joto atakuwa nje kwa mwezi mmoja kutokana na majeraha, kipa Alison Becker pia atakuwa nje.

Kiungo Curtis Jones naye ameumia hivyo atakuwa nje ya uwanja kwa muda ambao haujajulikana hadi sasa.

Wengine ni Dominic Szoboszlai na Alexander Trent Anord ambao ni majeruhi.

Habari Zifananazo

Back to top button