LIVERPOOL imepangwa kukipiga na klabu ya Spata Prague ya Jamhuri ya Czech katika hatua ya 16 mashindano ya Europa.
Droo iliyotolewa leo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya ( UEFA ) imeonesha AS Roma itakipiga na Brighton & Hove Albion.
West Ham itakipiga na Freiburg, AC Milan na Slavia Prague, Sporting Lisbon dhidi ya Atalanta.
Qarabag dhidi ya Bayer Leverkusen, wakati Benfica itavaana na Rangers.
Marseille itacheza na Villarreal.