Liverpool yaiadhibu vibaya United Anfield

LIVERPOOL imeibamiza Manchester United mabao 7-0 kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) katika mechi iliopigwa kwenye Uwanja wa Anfield Jumapili.

Cody Gakpo, Darwin Nunez na Mohamed Salah wote walifunga mara mbili na Roberto Firmino akafunga goli dakika za mwishoni, huku mabao sita kati ya hayo yakitokana na mchezo mkali wa kipindi cha pili.

Kipigo hicho kilikuwa kizito zaidi kwa Erik ten Hag kama meneja wa United na kuathiri sana harakati zake za kutafuta mataji, huku changamoto ya ubingwa wa Ligi Kuu sasa ikionekana kutowezekana.

Gakpo alianza kufunga dakika ya 43 baada ya Bruno Fernandes na Marcus Rashford kukosa nafasi na kuiweka Liverpool mbele.

Habari Zifananazo

Back to top button