Liverpool yamtambulisha Mac Allister

KLABU ya Liverpool imemtangaza rasmi kiungo Alexis Mac Allister kuwa mchezaji mpya wa timu hiyo.

Allister ambaye amesajiliwa kutoka Brighton amesaini kandarasi ya miaka mitano na anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na majogoo hao wa Anfield.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Argentina atavaa jezi namba 10 akiwa na timu yake mpya.

Advertisement