Lori chuma chakavu lafunga Barabara Bagamoyo

BAGAMOYO, Pwani: SHUGHULI za usafiri zimesimama kwa muda kuanzia saa 10 Alfajiri ya leo kutokana na ajali iliyotokea katika Barabara ya Bagamoyo, mkoani Pwani.

Mwandishi wetu ameshuhudia gari aina ya lori lililobeba vyuma chakavu likiwa limedondoka katikati ya barabara katika eneo la Kerege, wilayani Bagamoyo.

Ajali nyingine pia imetokea baada ya malori mawili kugongana katika eneo hilo la Kerege, hivyo kuwalazimu abiria wanaoisafiri kupitia barabara hiyo inayounganisha Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam, kutembea kwa miguu ili kuwahi katika shughuli zao.

Mpaka sasa askari wa usalama barabarani wanapambana ili kuruhusu huduma za usafiri kuendelea kama kawaida.

Habari Zifananazo

Back to top button