Lori la mafuta lashika moto Ruvu
KIBAHA, Pwani: MABASI mawili ya abiria moja likiwa mali ya kampuni ya Sauli luxury Bus linalofanya safari zake Dar es Salaam kwenda Mbeya na lingine mali ya kampuni ya New Force enterprises limited yamegonga lori la mafuta lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara eneo la Ruvu, Barabara Kuu ya Morogoro mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo muda mchache kabla ya ajali, lori hilo la mafuta liliharibika barabarani kabla ya basi la kampuni ya BM Coach kulipita gari jingine baadae dereva wa basi la Sauli kulifuata basi hilo bila kuchukua tahadhari jambo lililopelekea basi la New Force kufuata nyuma.
Shuhuda huyo ameendelea kueleza kuwa basi la Sauli liliparamia lori hilo lililokuwa pembezoni mwa barabara kabla ya basi la New Force kuligonga basi la Sauli kwa nyuma kisha kuwaka moto mda mfupi baadaye.
Bado hakuna taarifa rasmi kutoka Jeshi la Polisi juu ya tukio hilo la mapema leo asubuhi.