Lowassa alikuwa rafiki wa kweli-Millya

MBUNGE wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA), James ole Millya amesema marehemu Edward Lowassa alikuwa ni mtu mwenye urafiki wa kweli wakati wote.

Millya amesema hayo wakati akimzungumzia marehemu Lowassa ambaye alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu na aliyewahi kuwasaidia watoto wakike jamii ya wafugaji kusoma kwa bidii ili waje kuwa msaada mkubwa Kwa familia zao za kifugaji na jamii nyinginezo kwa ujumla.

“Mzee alikuwa ni mtu mwenye urafiki wa kweli bila unafiki, jamii imepoteza kiongozi ambaye itachukua muda kuziba pengo lake ”

Advertisement

Ameongeza kuwa jamii imepoteza kiongozi ambaye itachukua muda kuziba pengo lake maana alikuwa ni kiongozi mwenye udhubutu tutamkumbuka sana.