Lucia bosi mpya Red Cross

KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya  Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) chini ya Mwenyekiti wake David Kihenzile, imemteua Lucia Pande kuwa Katibu Mtendaji wa shirika hilo.

Awali,, Lucia alikua Makamu wa Rais wa shirika hilo.

Taarifa iliyotolewa leo Januari 8, 2023 inasema kuwa uteuzi wa Lucia kuwa Katibu Mtendaji kwa miaka mitatu umeanza leo  Januari 8 2023.

Advertisement

Uteuzi huo ni kwa mujibu wa sheria kipengele cha 37 (1) cha Kamati Kuu ya Taifa ya Shirika hilo (NEC)

Lucia, ambae ana uzoefu wa miaka 17 katika masuala ya uongozi, amewahi kufanya kazi katika Kampuni mbalimbali mbali kama Meneja Rasilimali Watu na usimamizi wa vifaa.

Baadhi ya Kampuni alizowahi kufanya kazi ni Tata Holding Ltd, Logistics, Dar es Salaam Corridor group, Kampuni ya madini ya Tanzanite One, Accasia na Barrick.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *