Ludewa wafurahia kung’ara Nanenane

HALMASHAURI ya Wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe imeshika nafasi ya kwanza kitaifa kwa mwaka 2023 katika maonesho ya Nanenane kupitia kundi la Halmashauri.

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Mwanziva amesema kwa ushindi huo, wilaya hiyo imetunukiwa tuzo na cheti cha pongezi.

Amesema kwa upande wa ufugaji wa samaki halmashauri hiyo imeshika nafasi ya pili kitaifa, ambapo mfugaji Longinus Mgani kutoka Kata ya Lugarawa, Tarafa ya Liganga Wilaya ya Ludewa ameshindanishwa na wafugaji wa halmashauri zingine na kushika nafasi hiyo ya pili na kutunukiwa Sh milioni sita na cheti cha pongezi.

Kupitia ushindi huo, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Mwanziva, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Sunday Deogratias, wataalam na watumishi wote wa Sekta ya Kilimo Wilayani hapo wamewashukuru Watanzania kwa kuwaunga mkono katika kipindi hicho cha Nanenane katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Habari Zifananazo

Back to top button