Lulandala:Tutatetea chama na viongozi wetu
KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM), Raphael Lulandala,amesema umoja huo una wajibu wa kukilinda chama na viongozi wake kwa wivu mkubwa bila kuogopa.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi mkoani Dodoma mara baada ya kupokelewa katika ofisi za makao makuu ya umoja huo mjini hapa.
“Hakuna sababu ya kuwa na katibu wa UVCCM kwenye wilaya zetu, kata zetu na mikoa kama chetu kinashambuliwa katika maeneo yao, ukiona mchungaji wa kondoo amepigwa lengo sio mchungaji ni kondoo,” alisema Lulandala.
Lulandala ameongeza viongozi wa UVCCM lazima kuwa mfano wa kuwatetea viongozi na kukilinda chama.