Lulu aonya mashabiki kuhusu kauli zao
MWIGIZAJI wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amewaomba mashabiki kuwa makini na baadhi ya kauli zao kwenye mitandao kuhusu wasanii, kwani baadhi ya kauli hizo zinawaumiza.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Lulu amesema kuwa wao pia wana ndugu, jamaa na marafiki ambao wanawaheshimu usimzungumzie kibaya kwa kuwa hata wao wanaumia.
“Binafsi ninamoyo na mtu akinizungumzia vibaya najisikia vibaya pia siwezi kuvumilia lazima nitajibu mashabiki zetu hata kama sio shabiki basi tuhesimiane.
” amesema Lulu
Pia ameongeza kuwa wanaumizwa na vitendo hivyo vya kusemwa na kukejeriwa mitandaoni.