MKUU wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba amesema kuwa hatarajii kuona Mkuu wa Wilaya anatumia nafasi yake kuwaweka ndani wananchi kimabavu na uonevu.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Tanga, James Kaji na kueleza kuwa hatarajii kuona wakuu wa wilaya wanatumia vibaya sheria ya kuwaweka watu ndani.

“Wakati wangu niwaombe mzingatie maadili ya kiongozi, ikiwemo kujiingiza kwenye makundi ambayo yatavunja heshima yako kama kiongozi, ikiwemo kutengeneza madeni ambayo huwezi kuyalipa,”amesema RC Kindamba.
Mkuu wa Mkoa amemtaka DC Kaji kusimamia mapato, kuhamasisha kilimo pamoja na kusimamia mgawanyo wa fedha za makundi maalum ya wanawake, vijana na wenye ulemavu.