‘Maabara Chuo cha Nelson Mandela ina uwezo mkubwa’

Mkuu wa Chuo cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela , Omari Issa amesema maabara ya chuo hicho, ina uwezo mkubwa wa  kupima vitu mbalimbali na kutoa majibu chanya kwa maendeleo ya nchi.

Omari amesema hayo jijjni Arusha akiwa anahitimisha ziara ya siku mbili ya kutembelea taasisi hiyo tangu alipoteuliwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo.

“Maabara hii ni kubwa na ina uwezo mkubwa wa kupima vitu mbalimbali, nami naahidi nitakutana na viongozi wenzangu ili kuangalia namna ya kuitumia maabara hii katika kupata majibu ya vipimo mbambali ikiwemo kushirikiana na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali,” amesema. 

Amewaagiza  wasimamizi wa maktaba katika chuo hicho kuhakikisha tafiti na bunifu mbalimbali zinazotolewa zinaingizwa kwenye kompyuta, ili vyuo vingine vya ndani na nje viweze kupata uelewa zaidi kuhusu Nelson Mandela.

“Lazima tafiti zinazofanywa hapa zilete fursa ya biashara na hivyo kusaidia katika kutimiza malengo ya chuo,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button