Maabara ya JKCI yatangazwa ubora duniani
DAR ESSALAAM: MAABARA ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) imepata ithibati ya kimataifa (ISO 15189:2012) ya kutambuka kama maabara bora duniani.
Ithibati hii imetolewa na Shirika la kimataifa la viwango (ISO) kama maabara inayoaminika katika vipimo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa JKCI Dk Peter Kisenge amesema hatua hiyo kubwa kwasababu vipimo vyao sasa vinaamini kitaifa.
“Inaamini katika kupima magonjwa na tafiti na hii ni historia kubwa ambayo taasisi imepata nimshukuru Rais Samia kwa kuwezesha ununuzi wa vifaa na wataalamu kwasababu wanapokuja kufanya ukaguzi wanaangalia eneo lililohusika, watu wanaofanya vipimo na vifaa wakiridhika unaweza kupata ithibati.
Aliongeza “Ni kitu kigumu maabara nyingi za Afrika Mashariki na kati hazipati ithibati kama nchi tumeandika historia kubwa sana.
Dk Kisenge ameeleza kuwa kutokana na kupata ithibati nchi yoyote inaweza kuleta vipimo na vikafanyika hapo hususani wale wanaofanya tafiti hata za kidunia.
Amesema hatua hiyo itaongeza mapato kwa taasisi na kuwasaidia wananchi wa chini kabisa wasioweza kulipia vipimo.
Aidha amefafanua kuwa maabara hiyo ina uwezo wa kupima magonjwa mengine ya kuambukiza na yasiyomambukiza huku wakitarajia kupata maabara kubwa zaidi.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa maabara JKCI, Emanuael Mgawo amesema maabara hiyo imepitia taratibu mbalimbali ambapo walianza na bodi ya ithibati ya maabara mbalimbali za kimataifa na katika michakato hiyo walianza hatua kwa hatua katika kila mapungufu walifanya marekebisho na hatimaye kupita.
“Tunashukuru kwa kukidhi viwango vya kimataifa na maabara hii ilianzishwa mwaka 2018 na mpaka sasa miaka sita imeweza kukidhi viwango Kwa ushirikiano mkubwa wa watumishi wa maabara wamefanya jitihada mbalimbali kukidhi viwango.