Maambukizi Covid-19 yapungua kwa 18.4%

Tanzania yang’ara chanjo ya Covid-19 Afrika

MAAMBUZIKI ya ugonjwa wa Covid-19 yamepungua kwa asilimia 18.4 katika kipindi cha Agosti 26 hadi Oktoba 7, mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Aifello Sichalwe katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya kuhusu mwenendo wa Covid-19 kwa kipindi cha Agosti 27 hadi Oktoba 7, mwaka huu.

Alisema kuwa katika kipindi cha Agosti 26 hadi Oktoba 7, mwaka huu jumla ya wagonjwa 478 walithibitishwa kuwa na maambukizi ikilinganishwa na wagonjwa 586 kuanzia Julai 30 hadi Agosti 26, mwaka huu sawa na upungufu wa asilimia 18.

Advertisement

4.

Alisema kuwa katika kipindi hicho hakukuwa na vifo ikilinganishwa na kipindi cha Julai 30 hadi Agosti 2022 ambapo kulikuwa na vifo vinne vilivyoripotiwa kutokana na ugonjwa huo.

Alichanganua watu waliothibitika kuwa na ugonjwa huo katika mikoa 17 katika kipindi cha Agosti 27 hadi Oktoba 07, 2022.

Kwa mujibu wa Dk Sichwale, mikoa hiyo ni Dar es Salaam watu (382), Mwanza (28), Arusha (23), Mara (8), Dodoma (5), Manyara (5), Morogoro (5), Lindi (4), Mbeya (4), Singida (3), Pwani (2), Kigoma (2), Katavi (2), Ruvuma (2), Mtwara (1), Kilimanjaro (1) na Tanga (1).

Alieleza kuwa jumla ya wagonjwa wanne  waliothibitika kuwa na Covid-19 walilazwa na wote walikuwa hawajapata chanjo ikiwa ni punguzo la wagonjwa wanne ukilinganisha na wagonjwa nane  waliotolewa taarifa kwenye tamko lililopita.