Maambukizi ya Covid yaongezeka

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kuna ongezeko la wagonjwa wa Covid-19 kutoka asilimia 4.1 hadi asilimia 5.5.

Kupitia taarifa yake ya salamu za Krismasi leo Disemba 24, Ummy amesema kuwa takwimu za wiki ya kwanza ya Mwezi Novemba 2022 zinaonesha kuwa Watu 1,154 waliopima Covid-19, kati yao Watu 47 walikuwa wanaugua Covid-19 huku takwimu za wiki ya pili ya Mwezi Desemba 2022 zinaonesha kuwa, kati ya Watu 1,294 waliopima Covid-19, watu 71 walikuwa wanaugua Covid-19.

“Wagonjwa wa Influenza wameongezeka kutoka asilimia 4.8% hadi asilimia 6.5% (kati ya watu 277 waliopima Influenza katika wiki ya kwanza ya Mwezi Novemba 2022, Watu 11 walikuwa wanaugua ugonjwa huo huku takwimu hizo hizo pia katika Wiki ya pili ya Mwezi Desemba zinaonyesha kuwa kati ya watu 155 waliopima, watu 10 walikuwa wanaugua ugonjwa wa Influenza.” amesema Ummy.

Waziri Ummy amesema Wizara ya Afya inakumbusha wananchi kuchukua hatua ili kujikinga na magonjwa haya ikiwemo kupata dozi kamili ya chanjo ya Covid – 19 kwa ambao hawajachanja, hatua hii itawaepusha kupata ugonjwa mkali wa Covid-19 na hata kifo”

“Kuvaa barakoa pindi mtu anapokuwa na dalili za mafua au kikohozi na awapo kwenye mikusanyiko, kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka mara kwa mara na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na kuzingatia kanuni za afya na usafi binafsi ikiwemo kujikinga kwa kitambaa au kiwiko cha mkono wakati wa kupiga chafya au kukohoa,” ameongeza Waziri Ummy.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
gate io
3 months ago

I may need your help. I tried many ways but couldn’t solve it, but after reading your article, I think you have a way to help me. I’m looking forward for your reply. Thanks.

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x