‘Maamuzi kesi za biashara yatolewe kwa wakati’

MAHAKAMA imetajwa kuwa na nafasi kubwa katika kujenga mazingira wezeshi ya biashara kwa kutoa maamuzi ya kesi za kibiashara kwa wakati, hivyo kuwavutia wengi kuja kuwekeza nchini.

Jaji wa Mahakama ya Rufani, Augustine Mwarija alisema hayo jijini hapa jana wakati akifungua kongamano la mazingira wezeshi ya kufanya biashara yanavyoweza kurahisishwa.

Akifungua kongamano hilo kwa niaba ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, Jaji Mwarija alisema mahakama ina nafasi kubwa ya kujenga mazingira wezeshi ya biashara iwapo itatoa maamuzi ya kibiashara kwa wakati hali itakayowezesha wafanyabiashara kuendelea na shughuli zao.

Pia itawavutia wafanyabi ashara wengi kuwekeza hapa nchini. Alisema kongamano hilo limeandaliwa na Chuo cha Mahakama Lushoto na ubalozi wa Uingereza.

“Hapa tunajadili ni masuala gani na jinsi gani tu nawezesha ufanyaji biashara, si ufanyaji biashara tu sasa kuna vituo jumuishi vya utoaji haki kwa mahakama ngazi zote kuwa pamoja, hilo linarahisisha wananchi kufika mahakamani.

Jaji wa Mahakama ya Rufani, Dk Gerald Ndika alisema mkutano huo unajumuisha majaji wa Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu na viongozi kutoka sekta za biashara, Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Dk Paul Kihwelo ambaye pia ni Jaji Mahakama ya Rufani alisema kuwa kongamano hilo hufanyika

kila mwaka kabla ya siku ya sheria. Pia kuwaweka pamoja wadau wa mahakama katika kuboresha mazingira ya biashara. “Katika utendaji kazi, eneo muhimu ni ushirikishwaji wa wadau katika mnyonyoro wa utendaji haki,”

alisema. Alitaja wadau hao kuwa ni pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wengine. Alisema kuwa moja ya mambo yanayosaidia uboreshaji wa mazingira ya biashara ni utendaji wa haki kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).

Alisema matumizi ya Tehama yamepunguza tatizo la rushwa mahakamani.

 

Habari Zifananazo

Back to top button