Maandalizi Pasaka mambo safi

MAANDALIZI ya tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika kesho katika viwanja vya Leader’s Club yamekamilika kwa asilimia mia na waimbaji wameanza mazoezi ya steji tayari.

Akizungumzia na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama, amesema maandalizi ya tamasha yamekamilika kwa msalimia mia moja ikiwemo kuwasili kwa waimbaji wa injili kuwasili nchini.

Aidha, Msama amesema tamasha hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari na Mawasiliano na Teknolojia, Nape Nnauye, ambaye atamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.

Advertisement

“Tamasha hili litakuwa mahususi ya kusherekea miaka miwili ya Rais Samia Suluhu kuingia madarakani na kusherekea sikukuu ya Pasaka”amesema Msama.

Hata hivyo, Msama amewataka watanzania kujitokeza kwenye tamasha hilo ambalo halitakuwa na kiingilio.

“Tamasha hili halitakuwa na kiingilio litakuwa bure,tunawaomba watanzania wajitokeze kwenye tamasha la pasaka kwa ajili ya kumsifu Mungu”amesema Msama