Maandalizi siku ya Kiswahili duniani yakamilika

WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Tabia Maulid Mwita amesema maadandalizi ya kuelekea maadhimisho Siku ya Kiswahili duniani yamekamilika.

Akizungumza siku ya leo, Julai 3, 2023 amesema maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika Julai 7, Zanzibar yataambana na shamla shamla mbalimbali ikiwemo muziki wa taarabu kutoka ndani na nje ya Tanzania.

“Lengo la kuadhimisha Siku ya Kiswahili ni kuieleza dunia kuwa chimbuko la Kiswahili ni Tanzania,” alisema waziri.

Maadhimisho hayo yalianza rasmi mwaka 2022 baada ya kutangazwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Novemba 23, 2021.

Kwa upande wake katibu mkuu wizara ya utamaduni, sanaa na michezo Saidi Yakubu amesema tamasha hilo litahdhuriwa na watu kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Ujerumani, Ghana, Kenya, Visiwa vya Comoro na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Kim
Kim
2 months ago

My last paycheck was $2500 for working 12 hours a week online. My sisters friend has been averaging 8k for months now and she works about 30 hours a week. I can’t believe how easy it was once I tried it out. The potential with this is endless.

This is what I do……….>>> https://goodfuture10.blogspot.com

Last edited 2 months ago by Kim
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x