ASKOFU Mkuu wa Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Donald Mtetemela na Askofu Mstaafu wa Jimbo la Tanga Phillip Bàdi wamenususurika kifo jijini Dodoma baada ya gari walilokuwa wamepanda kugongana na pikipiki.
Hata hivyo, mtu mmoja anahofiwa kufariki dunia kutokana na ajali hiyo
Maaskofu hao walifika Dodoma kuusindikiza mwili wa aliyekuwa Askofu wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa, George Chiteto aliyefariki jijini Tanga wakati akiongoza ibada ya mke wa askofu mwenzake.
Akitoa taarifa hiyo kwa waumini waliohudhuria ibada hiyo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha St John, Profesa Timotheo Simalenga alisema ajali hiyo ilitokea leo alfajiri wakati gari walilokuwemo.kugongana na pikipiki na kusababisha kifo cha mtu mmoja
Alisema kuwa dereva wa gari walilokuwemo maaskofu hao aaliyetdjea he’s jina moja Lwiwa alipata majeraha kutokana na vipande vya Kioo kumwangukia na kumkaa usoni, ambapo pia alipata jeraha kwenye jicho
Mmoja wa watu waliofika kwenye eneo la tukio, William Mbwana alisema ajali hiyo ilitokea saa kumi na moja kasoro alfajiri
Shuhuda huyo alishauri mamlaka husika kulipa kipaumbele suala la alama za barabarani ili kuepusha ajali.
Hata hivyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema: “Sina taarifa hizo, nitafuatilia.”