Mabadiliko tabianchi kuongeza magonjwa ya mlipuko

WAZIRI wa Afya ,Ummy Mwalimu amesema magonjwa ya mlipuko na vifo vinatarajiwa kuongezeka Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania kutokana na athari za mabadiliko ya tabinchi.

Ummy amesema hayo wakati wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) ambapo ameshiriki katika kikao cha mabadiliko ya tabianchi na afya ngazi ya mawaziri wa afya kutoka nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani unaoendelea Dubai ,Falme za Kiarabu.

Ummy ametaja magonjwa yatakayoongezeka kuwa ni magonjwa ya kuhara, malaria, dengue na magonjwa yasiyopewa kipaumbele kama usubi, chikungunya, kichocho, matende na magonjwa ya mfumo wa hewa.

Advertisement

“Magonjwa ya aina hii yanatarajiwa kuongezeka kutokana na ongezeko la joto na mvua kubwa au chache zinazoletelezea mafuriko au ukame katika maeneo mbalimbali nchini,Majanga kama ya mafuriko yameonekana kusababisha milipuko ya magonjwa ikiwemo kipindupindu na Homa ya matumbo ambapo asilimia 88 tu ya wakazi wa mijini ndiyo wanaopata huduma ya maji safi na salama na kwa upande wa vijijini ni asilimia 77 na watu wenye vyoo vya aina yoyote ni asilimia 98.

Aidha alisema majanga kama ya mafuriko yamepelekea kuharibu vyanzo vya maji na miundombinu iliyopo na kupelekea upungufu na hatimaye milipuko ya magonjwa.

“Tanzania kama moja ya nchi zinazoathirika na mabadiliko ya tabia nchi inaendelea kuchukua hatua za makusudi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuandaa mpango mkakati na miongozo ya kukabiliana na majanga haya katika sekta ya afya.

Vile vile amesema Wizara imeandaa mfumo wa taarifa unaoweza kubashiri uwezekano wa kutokea milipuko ya magonjwa ya milipuko sambamba na mabadiliko ya hali ya hewa ya kila siku.

Aidha ameeleza kuwa Wizara inatafuta fedha za kutekeleza Afua mbalimbali za kukabiliana na kuhimili mabadiliko ya tabia nchi kwa ushirikiano na mashirika ya kimataifa yanayojishughulisha na mazingira, Afya na maendeleo ya jamii.

Wakati wa mahojiano maalum na HabariLEO Daktari Bingwa wa Magonjwa ya ndani wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Elisha Osati amesema joto likiwa kali inasababisha watu kupoteza maji mengi mwili na damu kuwa nzito kutokana na kupoteza maji hivyo mtu anabaki na chumvichumvi na hivyo hali hiyo inaweza kuathiri figo,kupata shida kwenye ubongo kwa kupata kiharusi na mapigo ya moyo kwenda haraka.

“Kwenye ubongo sehemu inayochuja joto inaathrika kila joto inavyoongezeka na mwili itashindwa kufanya kazi kwani mwili unafanya kazi kwenye joto la 36 hadi 38 haitakiwi kuvuka mfano mazingira yanakuwa na joto ya chini kuliko mwili na kama mazingira yanajoto jingi mwili unashindwa kupoteza joto na jotoi la mwili linanda zaidi.

Amesema athari kwa watoto wadogo na wazee ni kubwa kwani miili yao imepungua mafuta ambayo yanasaidi kuongeza joto.

“Baridi pia ikiwa nyingi mwili unashindwa kufanya kazi zake na hapo inaweza fikia mtu akapoteza maisha kwa kupata tatizo linaloitwa Haipothemia baada ya joto kuwa la chini sana ,moyo kuathirika,”ameeleza Dk Osati.

“Kuna magonjwa yanayotokana na uharibifu wa mazingira vumbi nyingi inaathiri mapafu na njia ya hewa kwa maeneo ya vijijini kina mama wanalazimika kutumia mavi ya ng’ombe kama kuni moshi inawaathiri Kwenye mapafu wakati wa kupika na vumbi inaweza kuleta shida ya kukohoa na mapafu kushindwa kufanya kazi.

Pia amesema afya ya akili inaweza kuathirika kutokana na kupoteza maji inaathiri ubongo na kupoteza umakini ambapo hiyo hali inaleta msongo wa mawazo na baadae sonona na kama mtu alikuwa na hatari inaongezeka zaidi.

Dk Osati alisema endapo mtu ataathiriwa na joto ni vizuri akapelekwa hospitali endapo mabadiliko yataonekana na kama atahitaji kuongezewa maji ataongezewa kwaajili ya kupooza mwili.

Amesema kama ni baridi anapaswa kula vyakula vya moto na kujifunika mavazi yenye kuleta joto.
“ Ni muhimu kuepuka vinywaji kama pombe inatabia ya kutoa maji mengi na inachangi figo kufanya kazi haraka na kutoa maji mengi tunashauri mtu asinywe pombe sana wakati wa joto.

Aidha amesema wakati huu wa mvua kubwa watu wengine wanatumia nafasi ya mafuriko kutapisha vyoo hivyo umakini unahitajika katika mifumo ya mitaro kukaa sawa kama ni uchafu unaingia kwenye mfumo rasmi .
Habari hii imewezeshwa na MESHA na Ofisi ya Afrika ya IDRC Mashariki na Kusini.

12 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *