Mabadiliko tabianchi yatajwa kuathiri tiba asili

MAABARA ya Mkemia Mkuu wa Serikali imesema mabadiliko ya Tabianchi yana sababisha mabadiliko ya sifa na tabia ya mimea asili hali inayopunguza au kubadilisha sifa za dawa asili na kutokufanya kazi ipasavyo.

Akizungumza na HabariLEO jijini Dar Es Salaam Meneja wa Maabara ya Chakula na Dawa katika Mamlaka ya Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali(GLCA) Dk Shimo Peter alisema mabadiliko ya tabianchi ni kwamba sifa au tabia ya mimea inabadilika endapo mtu alitegemea mimea hiyo inampa kiwango fulani cha dawa na kumbe kutokana na mabadiliko imeshabadilika hawezi tena kupata ile dawa anayotarajia.

“Lakini pia unaweza ukawa unapata mimea hii katika mkoa huu au eneo imekufa yote na inapatikana katika maeneo mengine kwahi mabadiliko ya tabia nchi inasababisha sifa nyingi ya mimea kubadilika inaweza ikawa inazalisha dawa hii sasa inazalisha nyingine ,”amefafanua.

Amebainisha kuwa mabadiliko ya tabianchi yanaweza kusababisha matumizi mengine zaidi ya kupambana na vimelea ,kupambana na viuatilifu na vitu vingine ambayo inasababisha sifa za mimea kubadilika.

“ Kuhusu dawa asili na nafasi ya maabara ya mkemi mkuu katika hizi dawa kisheria dawa asili zinaratibiwa na kusajili na baraza la tiba asili na tiba mbadala katika taratibu za kusajili kuna sehemu muhimu ya kufanya uchunguzi kwa hizo dawa asili ili kuweza kuthibitisha ubora na usalama wa hizo dawa kabla hawajafanya maamuzi yoyote,”ameeleza.

Amesema mtu anaweza akatumia muda mrefu lakini kutokana na mabadiliko ya tabianchi na maendeleo kumekuwa na changamoto kubwa ya uchafuzi wa mazingira ndio maana wanawapa elimu sababu ya dawa kupimwa .

Aidha amesema wanapozungumzia ubora wa wanataka kubaini na kuona namna gani dawa zimetengenezwa ambapo wanaangalia viambata vya kemikali dawa ambazo zipo katika dawa.

Kwa upande wa usalama amesema wanaangalia kama hizo dawa hazina maambukizi ya vimelea ,hazina mabaki ya madini tembo ,hazina masalia ya viatilifu,hazina sumu kuvu lakini pia dawa hizo hazina mchanganyiko wowote na dawa zingine za kisasa kwani wapo watoa huduma ambao sio waaminifu wanakuwa wakitibu kutumia dawa asili ambazo zimechanganywa na dawa za kisasa.

“Kiwango cha watu kuja kupima dawa za asili kinaendelea kuongezeka na hii kutokana na watu kuwa na uelewa kwanini wapime pia inawasaidia kuweza kukidhi viwango vya ubora wa nchi lakini pia miongozo ya viwango vya kimataifa vya WHO(Shirika la Afya Dunaia) kuhakikisha vinakidhi viwango kuwa havina madhara kwa binadamu baada ya matokeo inawasaidia watafiti wengine kufanya tafiti zaidi kwa ufanisi wa dawa,”amesema.

Dk Peter aliwashauri watu kutumia dawa ambazo zimesajiliwa na baraza la tiba asili na mbadala kwasababu inakuwa imepita mchakato wote wa kuangaliwa usalama na ubora wake .

Pia aliwaasa watoa huduma wafanye kazi kwa kufuata miongozi na taratibu za serikali kuhakikisha dawa zao zimesajiliwa na wanatoa dawa ambazo zinaubora na usalama kwa jamii .

“Tunajua dawa zote zinamadhara baadae ikiwa utatumia bila kujua usalama wake na inaweza ukafanya wadudu au vimelea vikawa na usugu kwa kutumia dawa ambazo sio sahihi na dosi sahihi.

Habari Zifananazo

Back to top button