Mabadiliko ya ratiba yairejesha KMC Dar

KIKOSI cha KMC kimerejea Dar es salaam kikitokea Makambako kilipokuwa kimeweka kambi tangu Mei 18, kwa ajili ya michezo miwili ya Ligi Kuu Bara iliyosalia ambayo wataicheza mkoani Mbeya dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City.

Afisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema wamelazimika kurejea Dar baada ya kupokea taarifa ya mabadiliko ya michezo yao iliyosalia.

Kwa mujibu wa Mwagala wachezaji wa timu hiyo wamepewa mapumziko ya siku mbili na watarejea tena kambini siku ya jumatano kuanza maandalizi ya michezo hiyo ,na kisha kupanga upya taratibu za safari ya kwenda jijini Mbeya ambapo michezo hiyo inatarajiwa kupigwa Juni 6, dhidi ya  Tanzania Prisons na Juni 9, dhidi ya Mbeya city.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button