MABAO 23 yameingia kambani katika michezo minane ya raundi ya kwanza, siku ya kwanza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
–
Katika michezo hiyo, Barcelona amempa Royal mabao 5-0 katika dimba la Camp Nou.
–
Mchezo wa mapema AC Milan na Newcastle uliisha sare ya bila kufungana.
–
Manchester City ikiwa Etihad iliichapa Crvena mabao 3-1. PSG ikaichapa Dortmund mabao 2-0 uwanja wa Parc Des Princess.
–
Shaktar Donetsk ikiwa nyumbani ililala mabao 3-1 dhidi ya FC Porto. Feyernood akashinda mabao 2-0 dhidi ya Celtic.
–
Young Boys ikiwa nyumbani iliambulia kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa RB Leipzig, wakati Lazio wakiwa nyumbani wakaambulia sare ya mabao 1-1 dhidi ya Atletico Madrid.
–