Mabasi sasa ruksa kusafiri saa 24

DSM; SERIKALI ya Tanzania imeruhusu mabasi ya abiria kufanya usafirishaji wa saa 24, baaada ya kujiridhisha kiusalama, mwamko wa wananchi, huduma za mawasiliano pamoja na miundombinu ya usafirishaji.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchi, Jumanne Sagini wakati akizungumza na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na kusema kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya serikali kuimarisha shughuli za uchumi wa wananchi wake wa maeneo ya mjini na vijijini.

Pia amesema kwa kuzungatia maoni ya wadau mbalimbali wakiwemo wabunge, wamiliki wa mabasi, madereva wa mabasi, wasafiri, wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.

Pia serikali imetoa maagizo kwa wadau wote wa usafirishaji kuzingatia sheria, kanuni na utaratibu wa leseni zao, madereva kuthibitishwa na LATRA na kutoa ratiba za safari kwa saa 24.

Pia TANROADS kuhakikisha ubora wa miundombinu, serikali za mitaa kuhakikisha zinasimamia usalama wa abiria kwenye huduma wanazosimamia pamoja na Jeshi la Polisi kusimamia usalama wa watu na mali zao.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button